Ansar Dine wataka makundi mengine kuunga mkono juhudi za amani Mali
Kundi la Ansar Dine linaloshikilia sehemu ya eneo la Kaskazini mwa Mali lililoangukia kwenye mikono ya Makundi ya wailsam wenye msimamo mkali limetoa wito kwa makundi mengine kushiriki kwenye mazungumzo ya kisiasa.
Imechapishwa:
Mwakilishi wa Kundi la Ansar Dine Mohamed Aharid ambaye amekutana na msuluhishi wa mgogogoro huo ambaye ni rais wa Burkina Faso Blaise Compaore ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha hali ya kisiasa inarejea kama awali.
Katika tamko lililosomwa na mjumbe huyo, kundi hilo limetoa tamko la kusitisha uhasama, kuheshimu haki za msingi na uhuru wa binadamu, kuwarejesha watu wote waliokimbia makazi yao na wakimbizi na kutengeneza mazingira rafiki kwa ajili ya kutekeleza kikamilifu makubaliano ya amani ambayo ni chanzo kikuu cha mgogoro.
Kauli ya Ansar Dine inakuja kipindi hiki ambacho Wataalam wa Masuala ya Kijeshi kutoka Afrika, Marekani na Ulaya wakipanga mbinu za kupeleka Jeshi lao na hapa Ngari Gituku anaangalia kile kinachoendelea katika Taifa hilo.