Pata taarifa kuu
NIGERIA

Watu 363 wamepoteza maisha kwa mafuriko tangu mwezi Julai nchini Nigeria.

Watu mia tatu na sitini na tatu wamapoteza maisha nchini Nigeria na wengine milioni mbili na laki moja wamelazimika kuyahama makazi yao kutokana na mafuriko ambayo yameanza kuikumba nchi hiyo tangu mwezi Julai.  

Athari za mafuriko katika mji wa Abuja nchini Nigeria
Athari za mafuriko katika mji wa Abuja nchini Nigeria indiavision.com
Matangazo ya kibiashara

Kitengo cha Taifa cha kukabiliana na majanga nchini Nigeria kimetoa takwimu hizo na kueleza hali imezidi kuwa mbaya katika taifa hilo lenye idadi kubwa zaidi ya watu barani Afrika.

Mafuriko hayo yameacha athari kwa watu milioni saba na laki saba ambapo kati yao elfu kumi na nane na mia mbili na wawili wamejeruhiwa na mafuriko hayo ambayo yanatajwa kuwa mabaya zaidi kulikumba taifa hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.