Pata taarifa kuu
SYRIA

Mashambulizi ya mabomu yatatiza mpango wa makubaliano ya amani baina ya serikali na waasi nchini Syria.

Milipuko ya mabomu yaliyotegwa garini na risasi za moto ilitatiza makubaliano tete ya amani baina ya serikali na waasi nchini Syria saa chache tu baada makubaliano hayo kuanza ili kupisha sikukuu ya Eid al Haji.

Gari lilokuwa na bomu likiteketea baada ya kulipuka
Gari lilokuwa na bomu likiteketea baada ya kulipuka presstv.ir
Matangazo ya kibiashara

Vyombo vya habari vya taifa vimearifu kuwa watu nane wamepoteza maisha na wengine thelathini wamejeruhiwa kufuatia shambulio la bomu la kutegwa garini mjini Damascus huku waangalizi wa haki za binadamu wakiarifu kutokea kwa shambulio lingine katika mji wa Daraa, mashambulio yanayodaiwa kutekelezwa na waasi.

Waasi nao wanavituhumu vikosi vya serikali kwa kufanya mashambulizi ya risasi katika eneo la Kaskazini, ambapo waangalizi wa Haki za Binadamu nchini humo wakiarifu kutokea mapigano karibu na ngome muhimu ya kijeshi ya Wadi Deif.

Aidha jeshi la serikali limedai kuwa limefanya hivyo kujibu mashambulizi ya waasi walio vunja makubaliano ya kusitisha mapigano kupisha sikukuu ya Eid al Haji ambayo ilianza majira ya alfajiri.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.