Pata taarifa kuu
DRCONGO-UN

Umoja wa Mataifa wazituhumu Rwanda na Uganda kuendelea kuwaunga mkono waasi wa kundi la M23

Umoja wa Mataifa kwa mara nyingine tena umezituhumu Rwanda na Uganda. Katika ripoti iliotolewa na wataalamu wa Umoja wa Mataifa na kusema kwamba Kigali na Kampala zaendelea kuwaunga mkono waasi wa kundi la M23 licha ya serikali ya nchi hizo kuendelea kukanusha.

Vikosi vya Umoja wa Mataifa jijini Goma, Julay, 23, 2012.
Vikosi vya Umoja wa Mataifa jijini Goma, Julay, 23, 2012. REUTERS/James Akena
Matangazo ya kibiashara

Ripoti ya mwisho iliotolewa na wataalamu wa Umoja wa Mataifa imethibitisha kuwa serikali za Rwanda na Uganda zimeendelea kutowa msaada kwa kundi la waasi wa M23 katika mwezi Julay, Agosti na Septemba wakati nchi hizo zikituhumiwa na jamii ya kimataifa. Ripoti hiyo imesema kwamba serikali za nchi hizo zimewapa waasi wa M23 msaada wa kijeshi, ujasusi na ushauri wa kisiasa.

Wataalamu hao wamesema kundi la M23 limeendelea kujizatiti vya kutosha na kuwaajiri takriban watoto 250 katika jeshi lao.

Ripoti hiyo itawekwa hadharani mwezi Novemba na huenda ikaiweka serikali ya Rwanda katika hali ngumu kimataifa. Wawakilishi wa Rwanda kwenye Umoja wa mataifa wametuhumu mbinu za wataalamu hao ambao wamesema hawakuwaona viongozi wa serikali ya Rwanda kabla ya kutowa tuhuma hizo mpya.

Hayo yakiarifiwa, kaskazini mwa DRCongo, licha ya kutokuwepo mapigano baina ya wanajeshi wa serikali FARDC na wapiganaji waasi wa kundi la M23, hali bado ni tetea, hasa katika mji wa Goma ambako hali ya usalma mdogo inapelekea wananchi kuendelea kueshi katika hali ya hofu.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.