Pata taarifa kuu
UFARANSA

Serikali ya Ufaransa yatangaza bajeti yake ya mwaka 2013, matajiri kutozwa kodi zaidi

Waziri mkuu wa Ufaransa Jean-Marc Ayrault ametangaza bajeti mpya ya Serikali inayoongozwa na rais Francois Hollande huku ikishuhudiwa watu wanaopata mapato hadi kufikia euro milioni 1 wakipandishiwa kodi. 

Rais wa Ufaransa, Francois Hollande
Rais wa Ufaransa, Francois Hollande Reuters
Matangazo ya kibiashara

Bajeti hiyo itajumuisha kiasi cha euro bilioni 30 ambacho serikali ya Hollande imepanga kukikusanya kwa lengo la kukabiliana na deni la ndani ambalo limeendelea kuongezeka kutokana na mtikisiko wa kiuchumi.

Maofisa wa Serikali wamesema kuwa karibu robo tatu ya bajeti itategemea zaidi mapato yatakayotokana na kodi ambapo kwa mara ya kwanza matajiri watakuwa wanatozwa kodi kubwa zaidi ukilinganisha na watu wa kawaida.

Mbali na ongezeko la kodi kwa watu matajiri, bajeti hiyo pia ianlenga kukusanya kodi toka kwa wafanyabiashara wakubwa na makampuni ya kigeni ambayo yamekuwa yakifanya kazi zake nchini humo.

Suala jingine ambalo litajumishwa kwenye bajeti hiyo ni suala la ajira kwa vijana, suala ambalo limeonekana kuwa ni changamoto kubwa kwa Serikali ya rais Hollande ambayo imekuwa kwenye shinikizo kubwa la kutakiwa kutengeneza ajira.

Wachambuzi wa masuala ya uchumi wanasema kuwa bajeti hiyo inatarajiwa kuwa ni bajeti ya kwanza kwenye historia ya taifa hilo katika kipindi cha miaka ishirini ambayo itashuhudia ubanaji matumizi wa hali ya juu.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.