Pata taarifa kuu
KENYA-SOMALIA

Majeshi ya Kenya nchini Somalia yakiri kuua raia sita wa Somalia kimakosa kwenye mji wa Janay Abdalla

Majeshi ya Kenya nchini Somalia yamekiri kuwauwa raia sita kimakosa kwenye mji wa Janay Abdalla kilometa 50 toka mji wa Kismayo.

Msemaji wa majeshi ya Kenya nchini Somalia,  Cyrus Oguna
Msemaji wa majeshi ya Kenya nchini Somalia, Cyrus Oguna REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa msemaji wa majeshi ya KDF yaliyoko nchini Somalia, kanali Cyrus Oguna amekiri kuuawa kwa raia hao sita na mwanajeshi mmoja wa Kenya na kuongeza kuwa tayari maofisa usalama wanamshikilia kwa mahojiano mwanajeshi aliyetekeleza shambulio hilo.

Kanali Oguna hata hivyo amekanusha taarifa kuwa shambulio hilo lilitekelezwa kwa kudhamiria na kwamba wanalifanyia uchunguzi tukio hilo kwa kufanya mahojiani na askari ambaye alitekeleza shambulio hilo.

Awali majeshi hayo yalikanusha kuua raia hao mpaka pale taarifa hizo zilipothibitishwa kuwa waliouawa hawakuwa wapiganaji wa kundi la Al-Shabab kama ilivyoripotiwa hapo awali.

Hili linakuwa ni shambulio la kwanza kufanywa na wanajeshi wa Kenya dhidi ya raia toka kuanza kwa operesheni yao ya kuwasaka wapiganaji wa kundi la Al-Shabab ambao wameweka ngome yao kwenye mji wa Kismayo.

Operesheni kuelekea kwenye mji huo inaongozwa chini ya mwavuli wa majeshi ya AMISOM ambayo msemaji wake amesema uchunguzi kuhusu tukio lilolofanywa na wanajeshi wa Kenya linachunguzwa hivi sasa na aksari huyo amenyang'anywa silaha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.