Pata taarifa kuu
SYRIA-DAMASCUS

Viongozi wa upinzani nchini Syria wanaopinga uvamizi wa majeshi ya kigeni nchini humo wakutana mjini Damascus

Viongozi wa upinzani nchini Syria wanaopinga kutumika kwa nguvu za kijeshi nchini humo wamekutana kwa mazungumzo kwenye mji mkuu wa nchi hiyo Damascus na kutaka kundoka madarakani kwa rais Bashar al-Asad. 

Msuluhishi mkuu wa Mgogoro wa Syria, Lakhdar Brahimi (kushoto)
Msuluhishi mkuu wa Mgogoro wa Syria, Lakhdar Brahimi (kushoto) REUTERS/Khaled al-Hariri
Matangazo ya kibiashara

Mazungumoz hayo ya upinzani ambayo ni ya kwanza kufanyika kwenye mji mkuu wa nchi hiyo yalihudhuriwa na wawakilishi toka nchi za Iran, Urusi na China ambao ni marafiki wakubwa wa rais Asad.

Kwenye mkutano huo viongozi hao wa upinzani wametaka kuondoka madarakani kwa rais Asad lakini wameendelea kupinga uvamizi wa kijeshi toka kwa mataifa ya magharibi kufanya kazi hiyo wakisisitiza wataifanya kazi hiyo peke yao.

Mazungumzo hayo pia yamezitaka nchi za China na Urusi kuacha kumuunga mkono rais Asad kwa kile anchokifanya, kauli ambayo hata hivyo ilipata upinzani mkali toka kwa marafiki wa Syria.

Viongozi hao wameeleza wasiwasi wao iwapo rais Asad atatekeleza mapendekezo ya kusitisha mapigano na kukubali kuachia madaraka kwa njia ya amani jambo ambalo wamesema asipofanya hivyo basi vita vitaendelea nchini humo.

Wakati wa mkutano huo ulinzi mkali ulikuwa umewekwa mjini Damascus na viunga vyake kuhofia vitendo vya kigaidi ambavyo vingeweza kutekelezwa na makundi ambayo yanapinga mataifa ya Iran na China kushiriki kwenye mazungumzo hayo.

Katika hatua nyingine Umoja wa Mataifa umelaani mapigano ambayo yanaendelea nchini humo huku ikizilaumu pande zote mbili kwa kukaidi maazimio ya kutaka kuweka silaha chini kunusuru maisha ya watu wanaouawa kutokana na mapigano hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.