Pata taarifa kuu
NIGERIA

Shambulio la bomu laua wawili na kujeruhi 48 kwenye mji wa Bauchi nchini Nigeria

Mtu mmoja amejitoa muhanga kwenye mji wa Bauchi kaskazini mwa nchi ya Nigeria na kuua watu wawili na kujeruhi wengine zaidi ya arobaini na nane katika shambulio lililolenga kanisa. 

Wananchi wa Nigeria wakiondoka kwenye moja ya maeneo ambako mashambulizi yamekuwa yakitekelezwa
Wananchi wa Nigeria wakiondoka kwenye moja ya maeneo ambako mashambulizi yamekuwa yakitekelezwa Reuters
Matangazo ya kibiashara

Polisi kwenye mji huo wamesema kuwa mtu huyo ambaye alikuwa kwenye gari alijilipua punde baada ya maofisa wa usalama kulisimamisha gari lake kwa ukaguzi nje ya geti la kanisa la mtakatifu John ambapo watu walikuwa wakiingia kusali.

Msemaji wa Polisi kwenye mji huo T. Steven amewaambia waandishi wa habari kuwa hali ya usalama imerejea kwenye hali ya kawaida baada ya ulinzi kuimarishwa kwenye eneo hilo.

Mji wa Bauchi umekuwa ukilengwa na mashambulizi ya wapiganaji wa kundi la Boko Haram ambalo linataka eneo hilo kuwepo kwa utawala wa Sharia jambo ambalo linapingwa vikali na Serikali.

Polisi imelilaumu kundi la Boko Haram kwa kuhusika na shambulio hilo ingawa kundi hilo halijathibitisha lolote iwapo wamehusika kwenye shambulio hilo lililolenga kanisa.

Mpaka sasa watu zaidi ya 1400 wameuawa kutokana na mashambulizi ya kundi la Boko Haram toka mwaka 2010.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.