Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-MAREKANI

Shambulizi la kujitoa mhanga lasababisha vifo huko Kabul ikiwa muendelezo wa kupinga filamu inayodhalilisha Uislam

Shambulizi la kujitoa mhanga ambalo limetekelezwa na mwanamke nchini Afghanistan katika Mji Mkuu Kabul limesababisha vifo vya watu kumi na wawili ikiwa ni muendelezo wa matukio ya kupinga filamu iliyotengenezwa Marekani ikimdhihaki Mtume Muhammad SAW. Shambulizi hilo limetajwa kama la kulipiza kisasi cha kuonesha kutoridhishwa na utengenezaji wa filamu ambayo inadhalilisha uislam pamoja na kiongozi wa dini hiyo Mtume Muhammad iliyotengenezwa nchini Marekani na kusambaa kwenye mtandano wa YouTube.

Shambulizi la Bomu la kujitoa mhanga lililolenga busi Jijini Kabul limesababisha vifo vya watu kumi na wawili
Shambulizi la Bomu la kujitoa mhanga lililolenga busi Jijini Kabul limesababisha vifo vya watu kumi na wawili
Matangazo ya kibiashara

Vifo hivyo vya watu kumi na wawili vinafanywa takwimu kuonesha watu thelathini wameshauawa tangua kuanza kwa vuguvugu la maandamano la kupinga filamu hiyo ambayo ilisababisha kushambuliwa kwa ubalozi wa Marekani nchini Libya na kusababisha kifo cha balozi wake.

Mwanamke huyo alijitoa mhanga kwenye kundi la raia wa kigeni ambapo taarifa za Jeshi la Polisi linasema raia tisa wa kigeni wamepoteza maisha kwenye shambulizi hilo la kujitoa mhanga lililotekelezwa mapema asubuhi ya jumanne.

Shambulizi hilo la kujitoa mhanga limetekelezwa kwenye barabara kuu ambayo inaelekea Uwanja wa Ndege ambapo taarifa zinasema kuna uwezekano raia hao wa kigeni walikuwa njiani kwa ajili ya kusafiri kuondoka nchini Afghanistan.

Kundi la Hezb-i-Islami ambalo ni la pili kwa ukubwa ukiondoa Kundi la Wanamgambo wa Taliban ndilo limejinadi kutekeleza shambulizi hilo la bomu la kujitoa mhanga wakisema wanapinga kikudhi cha wakristo wenye msimamo mkali kumdhihaki Mtume Muhammad kupitia filamu yao.

Msemaji wa Kundi la Hesb-i-Islami Zubair Sidiqi amesema wamefanikiwa kutekeleza shambulizi hilo ambalo mwanamke aliyetekeleza anaitwa Fatima aliyetekeleza kazi yake kwa umakini mkubwa sana.

Filamu ambayo imesababisha hasira kwa waumini wa kiislam duniani kote inatambulika kwa jina la "Innocence of Muslims" inayodaiwa kutengenezwa na wakristo wenye msimamo mkali waliopo nchini Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.