Chama cha Republican chamuidhinidha rasmi Mitt Romney kupeperusha bendera katika mbio za uraisi
Chama cha Republican nchini Marekani kimemuidhinisha rasmi Mitt Romney kupeperusha bendera ya chama hicho katika mbio za uraisi wa nchi hiyo unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu ambapo atamkabili raisi wa sasa Barack Obama.
Imechapishwa:
Romney sambamba na mkewe walijumuika na wanachama wengine wa Republican ambao walijitokeza kwa wingi jimboni Florida kutoa shukurani zake kwa chama cha Republic.
Mitt Romney anatarajiwa kutoa changamoto kwa mpinzani wake kutoka chama cha Democratic raisi wa sasa wa taifa hilo Barack Obama katika uchaguzi mkuu wa raisi mnamo mwezi Novemba ambapo changamoto mbalimbali bado zimeelezwa kuikabili Marekani ikiwemo kuyumba kwa uchumi na tatizo la ajira.
Kabla ya kuidhinishwa kuwa mgombea rasmi wa Chama Cha Republican kwenye mkutano mkuu wa Chama hicho Romney alipaswa kuungwa mkono na wajumbe elfu moja mia moja na arobaini na nne ndiyo kupata ridhaa ya kuwa mgombea.
Nafasi ya Romney ilizidi kuwa kubwa baada ya baadhi ya wagombea kujiondoa kwenye mbio za kusaka kuteuliwa kuwa mgombea kupitia tiketi ya Chama Cha Republican kwenye uchaguzi wa baadaye mwaka huu.
Mkutano wa chama cha Republican ulikuwa ukisubiriwa kwa hamu ili kumbaini mgombea ambaye atapeperusha bendera ya chama hicho.