Pata taarifa kuu
GAMBIA

Wafungwa tisa wahukumiwa kifo kwa kupigwa risasi

Wizara ya mambo ya ndani ya nchini Gambia imesema wafungwa tisa waliohukumiwa adhabu ya kifo walitumikia adhabu hiyo kwa kufyatuliwa risasi baada ya rais wa nchi hiyo Yahya Jammeh kuapa kutekeleza hukumu hiyo mpaka ifikapo katikati ya mwezi Septemba kwa wafungwa wote waliohukumiwa adhabu ya kifo.

Raisi wa Gambia Yahya Jammeh
Raisi wa Gambia Yahya Jammeh IISD/Earth Negotiations Bulletin/Wikimedia Commons
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa ya wizara hiyo, wanaume 9 na mwanamke mmoja walifayatuliwa risasi jumapili juma lililopita baada ya kuhukumiwa kifo na rufaa zao kugonga mwamba.

Taarifa ya wizara hiyo imeonya kuwa Serikali haitavumilia vitendo vya uvunjwaji wa amani na uhatarishaji wa maisha ya watu, kuharibu mali havitavumiliwa nchini humo kwa sababu yeyote ile.

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binaadam la Amnesty international liliripoti kutolewa kwa adhabu hiyo dhidi ya wafungwa 9 siku ya jumamosi, siku moja kabla ya Serikali ya Gambia kutangaza kutekelezwa kwa adhabu hiyo, ikiwa ni siku chache baada ya ujumbe wa umoja wa Afrika kumtaka rais Jammeh atengue mpango wake wa kuwahukumu kifo wafungwa 47.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.