Pata taarifa kuu
UGIRIKI

Ugiriki yahaha kuzishawishi nchi zinazotumia sarafu ya Euro

Waziri mkuu wa Ugiriki, Antonis Samara anakabiliwa na changamoto kubwa ya kuwashawishi viongozi wa nchi zinazotumia Sarafu ya Euro, juu ya jitihada za nchi yake.

Reuters/John Kolesidis
Matangazo ya kibiashara

Antonis Samaras, ametoa wito kuomba kupatiwa muda zaidi wa kutekeleza masharti ya kubana Matumizi na kufanya mabadiliko wakati huu wakielekea katika mazungumzo ya kupatiwa Mkopo.

Samaras atakutana na Mweneyekiti wa Mawaziri wa Fedha katika nchi zinazotumia Sarafu ya Euro, sambamba na viongozi wa Ufaransa na Ujerumani, baadae juma hili.

Mazungumzo yao yatahusu juu ya kutathimini iwapo Ugiriki imechukua hatua za kutosha ili iweze kupata Mkopo wa Euro bilioni 31.5. ambapo Samaras atakuwa na kibarua kikubwa kuonesha kuwa inauwezo wa kutimiza Masharti ndani ya miaka miwili ili kupatiwa kitita hicho, ambapo pia atatoa ushawishi wa kupatiwa miaka miwili zaidi kutimiza hayo.

iwapo itashindikana kwa Ugiriki kupata mkopo huo, nchi hiyo italemewa na mzigo wa Madeni na huenda ikalazimika kujiondoa uanachama wa nchi zinazotumia sarafu ya Euro.

Samaras amesema wanachokihitaji ni muda zaidi wa kujiandaa kuinua uchumi wa Ugiriki haraka na kunyanyua pato lake, na kufafanua zaidi kuwa kupatiwa muda zaidi hakuna maana kupatiwa fedha zaidi isipokuwa wanabaki katika kutimiza majukumu yao na kutimiza masharti.

Waziri mkuu huyo amedai kuwa nchi yake imefanya uchaguzi unaodhihirisha kuwa mchakato wa mabadiliko umefanyika kwa kuundwa kwa Serikali mpya na kuwa sasa wanafanya jitihada za mabadiliko na Ubinafsishaji na kuongeza kuwa si vyema kwa baadhi ya watu kuwarudisha tena nyuma.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.