Pata taarifa kuu
Ethiopia

Waziri mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi aaga dunia

Waziri mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi, amefariki dunia baada ya kuugua kwa miezi kadhaa. Serikali ya Ethiopia imesema kuwa Zenawi amefariki jana katika hospitali nje ya nchi alikokua akitibiwa ingawa serikali haijatoa taarifa za undani kuhusiana na kifo hicho.

RFI
Matangazo ya kibiashara

Zenawi amefariki akiwa na umri wa miaka 57 na hakuonekana wazi kwa miezi miwili mpaka kifo kinamkuta katika hospitali moja mjini Brussels nchini Ubelgiji alikokua akitibiwa.

Taarfa hizo za serikali zimesema kuwa marehemu Zenawi alikua akiendelea vizuri lakini ghafla alikimbizwa katika chumba cha wagonjwa mahtuti na madaktari hawakufanikiwa kuokoa maisha yake.

Kwa mujibu wa katiba ya Ethiopia naibu waziri mkuu Hailemariam Desalegn atakaimu nafasi hiyo.

Zenawi alikua mwanasiasa akitoka kuwa muasi wa msituni na kuingia madarakani mwaka 1991 baada ya kumng'oa dikteta Mengistu Haile Mariam, aliyekuwa akishikilia madaraka.

Seriakli ya Zenawi ilitoa mamlaka kwa tawala za kimila na kikabila lakini madaraka makuu yalikuwa mikononi mwa serikali kuu ikiongozwa na waziri mkuu mwenyewe.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.