Pata taarifa kuu
Rwanda-DRCongo

Baraza la usalama la umoja wa mataifa laingiwa shaka katika hatua za kuunda jeshi la pamoja

Baraza la usalama la umoja wa mataifa UN laibua shaka katika hatua za kuunda jeshi la pamoja litakalofukuza makundi ya waasi mashariki mwa Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Baadhi ya wapiganaji waasi wa M23 wanaoendesha machafuko mashariki mwa DRC
Baadhi ya wapiganaji waasi wa M23 wanaoendesha machafuko mashariki mwa DRC AFP
Matangazo ya kibiashara

Balozi wa ufaransa katika umoja wa mataifa Gerard Araud amethibitisha taarifa na kusema kwamba pendekezo la jeshi la pamoja limeibua shaka kubwa katika baraza la usalama kwasababu ya kutofikiria tatizo si kuunganisha mipaka kati ya Rwanda na DRC lakini pia kufikia makubaliano ya kisiasa baina ya pande hizo.

Balozi huyo ameongeza kuwa kuunda jeshi hilo kutachukua kipindi cha miezi kadhaa na kugharimu sana kwakuwa hatua ya kuwachukua wanajeshi wa MONUSCO katika mpango wa umoja wa mataifa nchini DRC kutapunguza utendaji wa jeshi hilo katika kuwalinda raia.

Aidha balozi huyo alitoa wito kwa waasi wa M23 kukomesha mapigano na pande zote mbili ikiwemo watendaji wa nje ya taifa hilo kufikia makubaliano kukomesha mateso kwa raia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.