Pata taarifa kuu
KAMPALA-UGANDA

Museveni: Marais wa Rwanda na DRC kukutana tena baada ya wiki nne kuzungumzia suluhu ya mgogoro wa mashariki mwa Kongo

Wakuu wa nchi za maziwa makuu (ICGLR) waliokuwa wanakutana jijini Kampala nchini Uganda wamemaliza mkutano wao bila ya kupatikana kwa suluhu kuhusu kumaliza machafuko yanyoendelea mashariki mwa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC.  

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Rais Paul Kagame wa Rwanda(kushoto),Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda(Watatu kulia) na Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo wakiwa katika mkutano wa viongozi wan chi za Maziwa Makuu unaofanyika jijini Ka
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Rais Paul Kagame wa Rwanda(kushoto),Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda(Watatu kulia) na Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo wakiwa katika mkutano wa viongozi wan chi za Maziwa Makuu unaofanyika jijini Ka Picha kwa Hisani ya Ikulu ya Tanzania
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa tamko lililotolewa na mwenyeji wa mkutano huo rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni, amesema kuwa mkutano kati ya viongozi wa Rwanda na DRc umepangwa kufanyika tena baada ya wiki nne kupita.

Hapo jana marais wa Tanzania Jakaya Kikwete, rais wa Kongo Joseph Kabila, rais wa Rwanda Paul Kagame na rais wa Uganda Yoweri Museveni walikutana kwa saa chache kujaribu kuzungumzia mzozo unaoendelea mashariki mwa nchi hiyo.

Kushindwa kupatikana kwa suluhu ya mashariki mwa Kongo kumeendelea kuzusha hali ya sintofahamu kuhusu uhusiano kati ya nchi ya DRC na Rwanda ambapo serikali ya rais Joseph Kabila imeituhumu Rwanda kuwafadhili waasi wa M23 tuhuma ambazo zimekuwa zikikanushwa na serikali ya rais Kagame.

Akizungumza wakati wa kuhitimisha mkutano wa viongozi wa nchi kumi na moja za maziwa makuu, rais Museveni amesema kuwa viongozi wa nchi hizo watakutana tena baada ya wiki nne kujaribu kutazama namna ya kumaliza mzozo wa mashariki mwa kongo.

 

Regional leaders on Wednesday wrapped a meeting on a proposed neutral force for the east of Democratic Republic of Congo without a breakthrough on the issue, according to a statement.

"We will meet again in four weeks," summit host Ugandan President Yoweri Museveni told the 11-member International Conference on the Great Lakes Region (ICGLR), including the presidents of Rwanda and DR Congo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.