Pata taarifa kuu
SYRIA-JORDAN

Waziri mkuu wa Syria akimbilia nchini Jordan kuomba hifadhi na familia yake

Waziri mkuu wa Syria Riad Farid Hijab ameelezwa kuikimbia nchi yake na kukimbilia nchini Jordani akiwa na familia yake kuomba hifadhi, maofisa wa Serikali ya Jordan wamethibitisha.

Waziri mkuu wa Syria,  Riad Hijab aliyekimbilia nchini Jordan
Waziri mkuu wa Syria, Riad Hijab aliyekimbilia nchini Jordan Reuters
Matangazo ya kibiashara

Taarifa za kukimbia nchi yake kwa waziri mkuu Hijab, zimeripotiwa pia kwenye kituo cha taifa cha televisheni ya Syria ambacho kimedai kuwa kiongozi huyo amekimbia nchi yake muda mfupi baada ya kuachishwa kazi rais Bashar al-Asad.

Hijab anakuwa kiuongozi mwingine wa juu kwenye serikali ya Asad kukimbilia nchini Jordan kufuatia hapo awali maofisa kadhaa wa jeshi pamoja na marubani wa ndege za kivita kufanya hivyo.

Hata hivyo hakuna taarifa rasmi zinazoeleza sababu za kiongozi huyo kukimbia nchi yake japo imeelezwa kuwa ni kwasababu za kiusalama na pia kutofautiana na rais Asad katika kufanya maamuzi.

Riad Farid Hijab aliteuliwa na rais Asad kushika madaraka ya uwaziri mkuu mwezi June mwaka huu punde mara baada ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa ubunge ulioshuhudia chama tawala kikiendelea kusalia madarakani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.