Pata taarifa kuu
ALEPPO-SYRIA

Mapigano zaidi yameshuhudiwa kwenye mji wa Aleppo

Mapigano zaidi yameripotiwa kwenye mji wa Aleppo nchini Syria kati ya wanajeshi wa Serikali na wapiganaji waasi wa jeshi huru la Syria na kufanya hali kuwa tete zaidi kwenye mji huo.

wapiganaji wa waasi wakiwa kwenye eneo mojawapo kwenye mji wa Aleppo
wapiganaji wa waasi wakiwa kwenye eneo mojawapo kwenye mji wa Aleppo Reuters
Matangazo ya kibiashara

Vikosi vya waasi vimetangaza kuuteka karibu nusu ya mji wa Aleppo tuhuma ambazo zimekanushwa vikali na Serikali ya Syria kwa madai kuwa wanadhibiti eneo kubwa la mji huo.

Katika hatua nyingine kumetolewa picha za video zikiwaonesha wapiganaji waasi wakiwaua kwa kuwapiga risasi wafuasi wanaodhaniwa kuwa ni wa rais Asad baada ya kuwakamata kwenye mji huo.

Licha ya picha hizo kutolewa jumuiya ya kimataifa haijasema lolote kuhusu ukatili huo unaofanywa na wapiganaji wa jeshi huru la Syria kwa kuwakamata na kuwaua wapiganaji hao hadharani.

Msemaji wa msafara wa waangalizi wa Umoja wa Mataifa nchini Syria, Sausan Ghosheh  amesema hali ya mapigano inazidi kuwa mbaya zaidi kwakuwa hivi sasa hata waasi wameanza kutumia silaha nzitonzito kukabiliana na wanajeshi wa Serikali.

Hapo jana rais Bashar al-Asad amewapongeza wanajeshi wake kwa kuendelea kuonyesha utiifu kwenye Serikali yake kwa kuendelea kukabiliana na waasi ambao amewaita magaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.