Pata taarifa kuu
LONDON OLIMPIKI 2012

Pazia la michezo ya Olimpiki lafunguliwa London, Uingereza

Michezo ya Olimpiki inafunguliwa rasmi Ijumaa hii usiku katika uwanja wa kimtaifa wa Olmpic jijini London.Maelfu ya wachezaji pamoja na wageni mashuhuri wakiwemo marais tayari wamewasili kushuhudia ufunguzi wa michezo hiyo ambayo ni mikubwa zaidi duniani. 

RFI
Matangazo ya kibiashara

Mwaka 2008 michezo hii iliandaliwa jijini Beijing nchini China kabla ya Uingereza kupewa nafasi ya kuandaa michezo ya mwaka 2012 ambayo Uingereza inasema ni ya kihistoria.
 

Rais wa kamati ya kimataifa ya Olimpiki (IOC) Jacques Rogge amesema kila kitu kimekamalika na kinachosalia ni wanamichezo mbalimbali kuonesha uwezo wao katika michezo itakayokamilika baadaye mwezi ujao.
 

Watu elfu 80 wanatarajiwa kuhudhuria ufunguzi wa michezo hiyo, huku serikali ya Uingereza ikiihakikishia usalama wale wote wakaoshiriki katika michezo hiyo pamoja na mashabiki.
 

Katika hatua nyingine timu ya ulengaji shabaha kutoka Korea Kusini imevunja rekodi ya dunia katuika mchezo huo kwa kulenga shabaha kwa mikuki 216 na hvyo kupata alama 18 ambazo ni za juu zaidi kuwahi kupatikana katika mchezo huo.
 

Tangu mwaka 1984 Korea Kusini imeshinda medali 15 za dhahabu katika mchezo huo.
Im Dong-hyun, ambaye ana ulemavu wa macho ni miongoni mwa wacheaji wa Korea Kaskazini waliandikisha rekodi mpya na sawa na wachezaji wengine Dong-hyun, Kim Bubmin na Oh Jin-hyek katika kitengo cha wachezaji wengi.
 

Mataifa ya Afrika Mashariki pia yatashriki katika michezo hiyo huku Kenya ikitarajiwa kufanya vizuri katika mashindano ya riadha hasa yale ya masafa marefu.
Rfi Kiswahili itakuwa ikikujuza kwana yale yanayokea katika michezo ya Olimpiki hivyo kaa mkao wa kula.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.