Pata taarifa kuu
SYRIA-MALAYSIA

Malaysia kufunga ubalozi na kuwaondoa raia wake Syria

Waziri Mkuu wa Malaysia Najib Razak amewataka raia wa malaysia kuondoka nchini syria mara moja na kusitisha mipango kutokana na hali mbaya ya usalama inayoikabili syria kwa sasa.

Raisi wa Syria Bashar Al Assad ambaye utawala wake unapingwa na kutakiwa kuondoka madarakani
Raisi wa Syria Bashar Al Assad ambaye utawala wake unapingwa na kutakiwa kuondoka madarakani Reuters/Sana/Handout
Matangazo ya kibiashara

Kufuatia suala hilo serikali ya Malaysia imetangaza kufunga ubalozi wake nchini Syria baada ya hali ya usalama kuchafuka katika siku za hivi karibuni.

Takribani raia 140 wa Malaysia wapo nchini Syria,ambao ni wanafunzi,wataalamu,na wanadiplomasia watano akiwemo balozi ambaye anatarajiwa kurejea nyumbani wakati huu.

Mapigano makali yaliendelea baina ya majeshi ya serikali ya Syria dhidi ya waasi na kugharimu maisha ya watu 90 ambao walifariki katika maeneo yote yaliyokuwa na mapigano nchini humo.

Kwa mujibu wa shirika la msalaba mwekundu Zaidi ya watu 17,000 wamepoteza maisha tangu uasi uibuke dhidi ya serikali ya  raisi Bashar Al Assad mnamo mwezi march mwaka jana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.