Pata taarifa kuu
DRC-UGANDA

Mwanajeshi wa Umoja wa Mataifa MONUSCO auawa nchini DRC kufuatia kuzuka kwa mapigano makali

Mwanajeshi mmoja wa Jeshi la Umoja wa Mataifa linaloshika doria nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo MONUSCO raia wa India kwenye mapigano baina ya wanajeshi wasaliti na wale wa serikali kwenye mpaka wa karibu na Uganda.

Wanajeshi wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani nchini DRC MONUSCO ambao mmoja wao ameuawa kwenye mapigano
Wanajeshi wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani nchini DRC MONUSCO ambao mmoja wao ameuawa kwenye mapigano AFP / MARC HOFFER
Matangazo ya kibiashara

Mwanajeshi huyo raia wa India inaelezwa alijeruhiwa vibaya kwenye mapigano hayo ambayo yalizuka kwenye eneo la mpaka na kuchangia kuzsha hofu ya usalama kipindi hiki ambacho wananchi wanaendelea kukimbia makazi yao.

Msemaji wa MONUSCO Madnodje Mounoubai amethibitisha kutokea kwa kifo cha mwanajeshiwao na kusema alilengwa moja kwa moja na waasi hao na kilichochangia kifo chake ni majeraha aliyoyapata.

Kifo hiki kinakuja siku moja baada ya serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kutangaza kuanzisha mashambulizi dhidi ya Kundi la Waasi la M23 lililoweka kambi yake karibu na Mbuga za Virunga.

Msemaji wa Kundi la M23 Luteni Kanali Vianney Kazarama amesema wamefanikiwa kuwafurusha wanajeshi wa serikali na kuwarudisha nyuma na sasa wanashikilia Mji wa Bunagana.

Nao wakazi wa Mji wa Bunagana wamethibitisha eneo lao kushikiliwa na Waasi huku wakazi wengi wakikimbia kupisha mapambano na kuomba hifadhi katika nchi ya Uganda kwa kuwa ni karibu na eneo hilo.

Katika hatua nyingine wanajeshi zaidi ya mia sita wa DRC wanatajwa kukimbilia nchini Uganda baada ya kuibuka mapigano makali kutoka na Waasi wa Kundi la M23 na walipozidiwa nguvu wakaona bora waingie huko.

Msemaji wa Jeshi la Uganda Peter Mugisha amethibitisha wanajeshi hao wa DRC kukimbilia nchini mwao na wataamua nini cha kufanya kuweza kuwasaidia baada ya kushindwa kwenye mapambano dhidi ya Waasi wa M23.

Kundi la M23 linaloongozwa na Mbabe wa Kivita Jenerali Bosco Ntaganda limeendelea kuipa wakati mgumu serikali ya Rais Joseph Kabila katika eneo la Mashariki kutokana na kupanga na kutekeleza mapambano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.