Pata taarifa kuu
SUDAN

Rais Omar Bashir asema maandamano nchini mwake hayahusiani na mapinduzi katika mataifa ya kiarabu.

Rais wa Sudan Omar Hassan Al Bashir amekanusha madai kuwa maandamano yaliyodumu kwa siku kumi nchini mwake yana uhusiano na mapinduzi ambayo yameshuhudiwa katika nchi za kiarabu yaliyosababisha mabadiliko nchini Tunisia, Misri na Libya.

Rais wa Sudan Omar Al Bashir
Rais wa Sudan Omar Al Bashir Reuters/Mohamed Nureldin Abdallah
Matangazo ya kibiashara

Rais Bashir amesema kuwa maandamano nchini mwake ni ya kupinga sera ya kubana matumizi ambayo imekuwa ikipendekezwa na nchi hiyo na kwamba hata idadi ya walioshiriki ni ndogo.

Maandamano nchini Sudan yameendelea kushika kasi kila uchao tangu Juni 18 baada ya baada ya rais Bashir kutangaza hatua za kubana matumizi ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa kodi na kuondoa ruzuku ya mafuta huku waandamanaji wakisema kuwa hawataki kusikia sera ya kubana matumizi.

Mwaka 1964 maandamano ya umma yalisababisha kuangushwa kwa utawala wa kijeshi nchini humo.

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.