SYRIA
Zaidi ya watu 100 wauawa katika machafuko Syria
Takribani watu 100 huku theluthi mbili wakiwa ni raia wameuawa katika ghasia nchini Syria jumamosi wakati majeshi ya serikali yalipojibu mashambulizi,waangalizi wa haki za binadamu nchini humo wamethibitisha.
Imechapishwa:
Matangazo ya kibiashara
Nalo shirika la kutetea haki za binadamu lenye makazi yake Uingereza limedai raia 65 wameuawa katika shambulizi la mabomu ikiwemo familia ya watu 6 huko Deir Ezzor,mashariki mwa Syria.
Taarifa ya shirika hili ilieleza kuwa Wanajeshi kumi na tisa wameuawa katika mapigano dhidi ya waasi ambayo waasi 3 walifariki huku vikosi 10 vikijisalimisha silaha walipojaribu kuwakabili majeshi yanayopinga serikali.