Pata taarifa kuu
MOSCOW-URUSI

Ufaransa yataka nchi ya Iran kuwekewa vikwazo zaidi baada ya mazungumzo ya Moscow kutotoa majibu muafaka

Serikali ya Ufaransa kupitia kwa waziri wake wa mambo ya nchi za nje Laurent Fabius imetaka kuchukuwa kwa hatua kali zaidi dhidi ya serikali ya Iran iwapo itaendelea na msimamo wake wakutotaka vinu vyake kukaguliwa.

Viongozi wa nchi sita zilizokuwa zikishiriki mazungumzo na Iran mjini Moscow kuhusu mpango wake wa Nyuklia na kumalizika bila ya maazimio
Viongozi wa nchi sita zilizokuwa zikishiriki mazungumzo na Iran mjini Moscow kuhusu mpango wake wa Nyuklia na kumalizika bila ya maazimio REUTERS/Kirill Kudryavtsev/Pool
Matangazo ya kibiashara

Waziri huyo amesema kuwa ni lazima Umoja wa Mataifa utangaze vikwazo zaidi dhidi ya Serikali ya Iran kuhusu mpango wake wa siri wa kurutubisha Nyuklia kwa matumizi ya kutengeneza silaha za maangamizi.

Kauli ya Ufaransa inakuja kufuatia hapo jana nchi sita zilizokuwa zikishirikia mazungumzo na Iran mjini Moscow Urusi, kumaliza mazungumzo yao pia ya kutoka na maazimio kamili kuhusu hatua walizoafikiana.

Hapo jana viongozi wote hawakusema chochote kuhusu kile ambacho kimekubaliwa na nchi wanachama kuhusu mpango wa Iran wala Iran yenyewe kusema chochote kuhusu walichoafikiana.

Mazungumzo ya mjini Moscow yalilenga kuishawishi nchi Iran kukubaliana na maazimio ya tume ya Umoja wa Mataifa inayosimamia masuala ya Nyuklia ambay ilitaka nchi ya Iran bila masharti kukubali vinu vyake kukaguliwa.

Viongozi wa Iran wenyewe wameendelea kusisitiza kuwa nchi yao haitumii nyuklia kutengeneza silaha za maangamizi kama inavyodaiwa na baadhi ya mataifa ya magharibi.

Kiongozi wa ujumbe wa Iran kwenye mazungumzo hayo, Saeed Jalili amesema mazungumzo yalikuwa ya umakini mkubwa lakini haki ya kurutubisha Nyuklia ni haki ya Iran na haipaswi kunyang'anywa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.