Pata taarifa kuu
Iarq

watu zaidi ya sitini wauawa nchini Iraq katika matukio tofauti

mahujaji wa kishia na polisi zaidi ya sitini wameuawa katika mashambulizi tofauti ya kujitowa muhanga yaliotokea leo jijini Bghdad nchini Iraq. Duru za polisi na hospitali zaarifu kuwa watu zaidi ya sitini wameuawa na wengine zaidi ya sabini wamejeruhiwa wakati waislam wa madhehebu ya kishia walipokuwa katika ibada yao muhimu.

Mashambulio ya kuvizia jijini Bagdad
Mashambulio ya kuvizia jijini Bagdad REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Licha ya wanajeshi wa Marekani kuondoka nchini humo, Iraq imekuwa ikishuhudia mashambulizi ya kuvizia ya kidini ambapo takwimu inazidi kuwa kubwa zaidi kuliko mwaka 2006-2007 wakati ambapo nchi hiyo ilikuwa katika hatari ya kutumbukia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Makundi ya waislam wa madhehebu ya kishia yenye mfungamano na Al Qaeda yamekuwa yakiwalenga waislam wa madhehebu ya kishia kwa kuwashambulia.

Jumatano hii ma bomu manne ya kutegwa yaliwalenga waislam wa madhehebu ya washia waliokuwa katika ibada ya kumkumbuka Imam wa kichia Moussa Al Kadhim jijini Bagdad, watu 18 waliuawa papo hapo.

Moja kati ya ma bomu hayo lililipuka wakati mahujaji hao wa kishia walipofika kwenye kituo cha polisi katika mwa jiji la Bagdad, lingine lililipuka wakati mahujaji hao waliokuwa katika harakati za kukusanya chakula.

Viongozi wa Iraq walizidisha ulinzi wiki hii jijini Bagdad wakati maelfu ya mahujaji wakitarajiwa kukusanyika katika kaburi la Imam Moussa katika mji wa Kadhimiah

katika mji wa Hilla wenye wakaazi wengi wa kishia, gari mbili zililipuka kwenye mgahawa unaotumiwa sana na polisi na kuwauawa 22 huku 38 wakijeruhiwa.

Matukio mengine yameshuhudiwa katika mji wa Balad ambako watu wanne wameuawa, na mjini Kerbala watu watatu wameuawa na wengine 17 wamejeruhiwa, na mtu mwingine ameuawa katika mji wa Hassoua na wengine wanne wameruhiwa kwenye umbali wa kilometa hamsini na jiji la Bagdad.

Homa ya joto la kisiasa imepamba moto licha ya uwepo mkataba wa ugavi madaraka baina ya washia na wa kurde. Waziri mkuu Nouri Al Malik analaumiwa kwa kosa la kuongoza nchi bila ushirikiano na viongozi wengine.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.