Pata taarifa kuu
SYRIA

Jeshi Huru la Waasi nchini Syria latoa saa 48 kwa serikali huku Baraza la Usalama likikumbwa na hofu ya kutokea mauaji zaidi

Wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UN wamekumbwa na hofu ya uwepo wa maelekezo ya kuendelea kwa machafuko nchini Syria huku Jeshi Huru la Upinzani likitoa saa arobaini na nane kwa serikali ya Rais Bashar Al Assad kutekeleza mpango wa kumaliza umwagaji wa damu uliopendekezwa na Mpatanishi wa Kimataifa Kofi Annan.

Wapiganaji wa Jeshi Huru la Upinzani nchini Syria ambao wametoa saa 48 kwa serikali kusitisha mauaji kwa raia kabla hawajaanzisha mapigano
Wapiganaji wa Jeshi Huru la Upinzani nchini Syria ambao wametoa saa 48 kwa serikali kusitisha mauaji kwa raia kabla hawajaanzisha mapigano Reuters
Matangazo ya kibiashara

Hofu ya wanachama wa Baraza la Usalama imeongezeka baada ya kuelezwa kwa ufupi hali inayoendelea nchini Syria kwa sasa na Naibu wa Annan, Jean Marie Guehenno ambaye pia ameweka wazi wamegundua miili kumi na mitatu ya watu waliouawa Mashariki mwa nchi hiyo katika Mji wa Assukar.

Guehenno amesema miilihiyo imekutwa ikiwa imefungwa kamba kwenye mikono na kufungwa kwa nyuma kitu ambacho kinadhihirisha watu hao waliuawa kwa kupigwa risasi na watu waliokuwa karibu yao kitu ambacho kinazidisha hofu kwa usalama wa wananchi.

Naye Kiongozi wa juu wa Jeshi Huru la Upinzani nchini Syria Kanali Qassim Saadeddine ametoa muda huo kwa serikali kupitia kanda ya video ikiutaka Utawala wa Rais Assad kutekeleza mara moja kuacha kutekeleza mauaji dhidi ya raia, kuondoa vikosi vyake na vifaru kwenye majiji na vijiji.

Kanali Saadeddine amesema Jeshi lake linasubiri hadi mchana wa ijumaa na kama serikali ya Rais Assad ikishindwa kutekeleza mapendekeo hayo wao hawatokuwa na uvumilivu tena na badala yake watavunja utekelezaji wa mpango wa Annan wenye lengo la kumaliza umwagaji wa damu uliodumu kwa miezi kumi na mitano.

Kiongozi huyo wa Jeshi Huru la Upinzani nchini Syria Kanali Saadeddine ameongeza serikali inatakiwa iruhusu huduma za kibinadamu ziwafikie waathirika wa machafuko yanaendelea nchini humo na pia utawala ufanye makubaliano na Umoja wa Mataifa UN ili kukabidhi madaraka kwa wananchi.

Licha ya haya yote kuendelea kutikisa suala la usalama nchini Syria lakini Balozi wa Urusi kwenye Umoja wa Mataifa UN Vitaly Churkin ameita hali ya kisiasa huko Damascus ni ya kusikitisha lakini amekiri kuna hatua chanya ambazo zimeshapigwa na kuleta matumaini ya kufikiwa muafaka.

Churkin hakusita kuzitaka pande ambazo zinahasimiana kuketi chini kwa ajili ya mazungumzo ambayo yatasaidia kutekelezwa kwa mapendekezo sita ambayo yalitolewa na Mpatanishi wa mgogoro wa Syria kutoka Umoja wa Mataifa UN na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu Kofi Annan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.