Pata taarifa kuu
SYRIA

Clinton na Ban wahofia kuibuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton ameishukia Urusi na kuituhumu sera zake za kupinga mapendekezo ya Umoja wa Mataifa UN kushukua hatua dhidi ya Syria inaweza kuchangia kuzuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe kwenye nchi hiyo iliyo kwenye machafuko kwa miezi kumi na tano.

Athari za mashambulizi na matukio ya kujitoa mhanga yanayoendelea kutamalaki nchini Syria na kuonekana kitisho cha kuzuka vita vya wenyewe kwa wenyewe
Athari za mashambulizi na matukio ya kujitoa mhanga yanayoendelea kutamalaki nchini Syria na kuonekana kitisho cha kuzuka vita vya wenyewe kwa wenyewe REUTERS/Shaam News Network/Handout
Matangazo ya kibiashara

Kauli ya Clinton imeungwa mkono na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Ban Ki Moon ambaye amesema Urusi imekuwa mstari wa mbele kupinga mapendekezo ya Umoja huo hali ambayo inaendelea kuweka Syria pabaya na huenda ikaingia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Clinton amesema Urusi imemweleza nia yake ni kudhibiti kuzuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe katika nchi ya Syria lakini yeye akawaeleza kutokana na kitendo chao cha kupinga mapendekezo ya Umoja wa Mataifa UN kitachangia kwa kiasi kikubwa kwa nchi hiyo kuingia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Waziri huyo wa Mambo ya Nje wa Marekani ameweka bayana sera zozote ambazo zinapinga maamuzi au mapendekezo ya Umoja wa Mataifa UN kuchukua hatua dhidi ya nchi ya Syria kunaiweka kwenye hatari ya kuibuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Kauli ya Clinton ameitoa akiwa kwenye ziara yake nchini Denmark ambapo ameendelea kuonesha hofu yake ya kutokea vita vya wenyewe kwa wenyewe iwapo Urusi itaendelea kusimamia kwenye sera zake za kuunga mkono kunachofanywa na serikali ya rais Bashar Al Assad.

Naye Katibu Mkuu wa UN Ban amesema iwapo mapendekezo yaliyotolewa na Mpatanishi wa Umoja wa Mataifa UN na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu Kofi Annan hayatatekelezwa ni wazi kabisa nchi hiyo itaingia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Ban amesema anaiomba serikali ya Syria kuhakikisha inatekeleza mapendekezo sita yaliyotolewa na Mpatanishi Annan ili kuiepusha nchi hiyo isiingie kwenye janga baya la vita ambavyo vitachangia vifo zaidi.

Wakati Ban anapendekeza kutekelezwa kwa mapendekezo sita ya Mpatanishi Annan nchi ya China ambayo ni rafiki wa Syria imesema mapendekezo hayo yanahitaji muda zaidi ili yatekelezwe na si kwa shinikizo la aina yoyote.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.