Pata taarifa kuu
MALI

Wajumbe wa kambi ya ECOWAS waondoka Mali

Wajumbe wawili wa umoja wa mataifa ya Afrika magharibi wameondoka nchini Mali jumamosi baada ya kushindwa kufikia muafaka na viongozi wa mapinduzi kupata kiongozi wa serikali ya mpito.

Kiongozi wa Junta nchini Mali kapteni Amadou Sanogo
Kiongozi wa Junta nchini Mali kapteni Amadou Sanogo Reuters/Luc Gnago
Matangazo ya kibiashara

Mjumbe wa kanda hiyo kutoka Burkina faso Djibril Bassole na kutoka Cote d'Ivoire Adama Bictogo wamekuwepo nchini Mali tangu jumanne kuwakilisha jumuiya ya kiuchumi ya afrika magharibi Ecowas katika mazungumzo na lililokuwa jeshi la Junta juu ya kutatua mgogoro wa kisiasa nchini humo.

Kabla ya kuondoka Mjumbe kutoka Cote d'Ivoire Adama Bictogo alisema mazungumzo na serikali ya Junta ambao walifanya mapinduzi march 22 kuhusu wadhifa wa kiongozi wa mpito yaligonga mwamba na kuwalazimu kuondoka nchini Mali.

Bictogo aliongeza kuwa kwa mujibu wa katiba ya kanda ya afrika magharibi inaaminika kuwa kiongozi wa sasa wa serikali ya mpito Dioncunda Traore angeweza kuendelea na wajibu kwa kipindi cha kwanza cha siku 40 lakini uongozi wa Junta haujakubaliana na jambo hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.