Pata taarifa kuu
MISRI-CAIRO

Mahakama nchini Misri yatoa hukumu kusitisha kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa Urais

Mahakama nchini Misri imetoa amri ya kuahirishwa kwa Uchaguzi wa Urais ambao ulipangwa kufanyika baadae mwezi huu, chanzo cha habari cha mahakama kimethibitisha. 

Viongozi wa kijeshi ambao wanatakiwa kuachia madaraka kwa Serikali ya Kiraia
Viongozi wa kijeshi ambao wanatakiwa kuachia madaraka kwa Serikali ya Kiraia Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mahakama ya mjini Benha nchini humo imesema Duru ya kwanza ya uchaguzi iliyopangwa kufanyika Tarehe 23 na 24 mwezi huu haitafanyika, kwa kuwa sheria haitoi mamlaka kwa mkuu wa tume ya uchaguzi kuitisha uchaguzi.

Amri hiyo ya mahakama itakatiwa Rufaa hii leo jijini Cairo, huku kukiwa na matumaini kuwa Uchaguzi huo utafanyika kama inavyotarajiwa.

Taratibu za kuelekea uchaguzi zimekuwa zikiyumbayumba kutokana na taratibu za kisheria ambazo zimeweka nchi hiyo katika hali ya sintofahamu.

Kiongozi wa kijeshi nchini Misri, Husssein Tantawi aliyeshika madaraka baada ya kuanguka kwa utawala wa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Hosni Mubarak ameahidi kukabidhi madaraka kwa yeyote atakayechaguliwa kuliongoza taifa hilo.

Hukumu ya mahakama hiyo huenda ikazusha tafrani miongoni mwa vyama vya upinzani na wananchi nchini humo ambao wanataka kuona uchaguzi unafanyika mwaka huu kwa lengo la kumaliza utawala wa kijeshi.

Wachambuzi wa mambo wanadai kuwa endapo uchaguzi huo hautafanyika mwezi huu, basi nchi hiyo itarajie kushuhudia maandamano makubwa ya nchi nzima kupinga uchaguzi huo kusogezwa mbele.

Kwa majuma mawili mfululizo maelfu ya wananchi nchini Misri wamekuwa wakiandamana kushinikiza kujiuzulu kwa Serikali ya kijeshi, Serikali ambayo imeahidi kuondoka madarakani mara baada ya uchaguzi mkuu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.