Pata taarifa kuu
UKRAIN

Yulia Tymoshenko apelekwa hospitali baada kuendelea kuwa kwenye mgomo wa kula

Mamlaka nchini Ukrain zimesema kuwa aliyekuwa waziri mkuu wa nchi hiyo Yulia Tymoshenko amepelekwa hospitalini kupatiwa matibabu baada ya kuendelea na mgomo wake wa kula. 

Aliyekuwa waziri Ukrain, Yulia Tymoshenko
Aliyekuwa waziri Ukrain, Yulia Tymoshenko Reuters
Matangazo ya kibiashara

Awali Tymoshenko alikuwa kwenye mgomo wa kula kushinikiza kutendewa haki ikiwemo kusikilizwa upya kwa rufaa yake aliyoikata kuhusu huku dhidi yake ya kutumikia jela miaka saba.

Viongozi mbalimbali wa Umoja wa Ulaya wameendelea kuongeza shinikizo kwa Serikali ya Ukrain kumuachilia huru kiongozi huyo wakidai hukumu yake imechochewa kisiasa.

Hivi karibuni mawakili wa Tymoshenko walidai kuwa mteja wao amekuwa akifanyiwa vitendo vya unyanyasaji kwenye gereza ambalo anashikiliwa ambapo pamoja na mambo mengine amekuwa akipigwa na maofisa wa gereza.

Hapo jana nchi hiyo ilitangaza kufuta kufanyika kwa mkutano wa 18 wa viongozi wa nchi za Umoja wa Ulaya baada ya mataifa kadhaa kutishia kutohudhuria mkutano huo kutokana na kushinikiza haki kwa Tymoshenko.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.