Pata taarifa kuu
UFARANSA

Ni Francois Hollande, mshindi wa kiti cha urais nchini Ufaransa baada ya kumuangusha Nicolas Sarkozy

Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Ufaransa, Francois Hollande amefanikiwa kushinda nafasi ya urais wa nchi hiyo kufuatia kumuangusha rais Nicolas Sarkozy kwenye uchaguzi wa duru ya pili nchini humo.

François Hollande, mshindi wa kiti cha urais nchini Ufaransa
François Hollande, mshindi wa kiti cha urais nchini Ufaransa REUTERS/Philippe Wojazer
Matangazo ya kibiashara

Hollande amefanikiwa kushinda uchaguzi huo wa duru ya pili baada ya kupata ushindi wa asilimia 51.67 ya kura zoet zilizopigwa wakati mpinzani wake Nicolas Sarkozy akipata asilimia 48.33 ya kura.

Mara baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo rais Nicolas Sarkozy akihutubia maelfu ya wafuasi wake kwenye kambi yake, amesema kuwa amekubali kushindwa na kwamba uteuzi walioufanya wananchi ni kutokana na mapenzi yao na anamtakia kila laheri mpinzani wake.

Kwa upande wake rais mteule Francois Hollande akihutubia wafuasi wake kwenye mji wake wa nyumbani, amewaahidi kufanya mabadiliko makubwa kwenye serikali ya nchi hiyo na kubwa akidai ni mabadiliko kwenye sera za Umoja wa Ulaya kuhusu uchumi.

Kiongozi huyo amewaonya viongozi wengine wa Umoja huo kuwa hatua ya ubanaji matumizi ili kukabiliana na mdororo wa uchumi sio suluhisho kwa jinsi hali ilivyo hivi sasa na kudai kuwa serikali yake itahakikisha inaachana na mpango huo.

Kiongozi huyo toka chama cha kisocialist anakuwa kiongozi mwingine wapili kuwa rais wa Ufaransa katika kipindi cha miaka 20 iliyopita.

Kwa mujibu wa wizara ya mambo ya ndani abayo ndio ilikuwa inasimamia uchaguzi huo imesema kuwa watu milioni 46 walijiandikisha kupiga kura ambapo asilimia 76 walipiga kura na kuwa rekodi ya kwanza kuwahi kuwekwa na wananchi wa taifa hilo kushiriki uchaguzi mkuu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.