Pata taarifa kuu
CHINA-MAREKANI

Mwanaharakati wa Haki za Binadamu Nchini China Guangcheng na familia yake wataka kuishi uhamishoni Marekani

Mwanaharakati wa Haki za Binadamu nchini China mwenye ulemavu wa macho Chen Guangcheng ameiomba serikali ya Marekani kumpa hifadhi yeye pamoja na familia yake baada ya kukamilika kwa mpango wa yeye kuondoka Ubalozi wa nchi hiyo huko beijing baada ya kujihifadhi kwa siku sita. Guangcheng amesema anaona bora akaishi uhamishoni nchini Marekani badala ya kuendelea kusalia nchini China ambako anahofu na usalama wake pamoja na familia yake kwani amekuwa akiandamwa na serikali na ndiyo sababu ya kumpa kifungo cha nyumbani alichokikimbia.

Mwanaharakati wa Haki za Binadamu Nchini China Chen Gaucheng akiwa katika Hospital ya Beijing anakopatiwa matibabu baada ya kutoka Ubalozi wa Marekani alikopewa hifadhi
Mwanaharakati wa Haki za Binadamu Nchini China Chen Gaucheng akiwa katika Hospital ya Beijing anakopatiwa matibabu baada ya kutoka Ubalozi wa Marekani alikopewa hifadhi AFP PHOTO/Jordan Pouille
Matangazo ya kibiashara

Mwanaharakati huyo ameweka wazi kuwa haamini ahadi iliyotolewa na serikali ya Beijing kuwa itampatia ulinzi wa uhakika yeye pamoja na familia yake baada ya matibabu yake kukamilika kutekeleza mkataba uliofikiwa baina yao na Marekani.

Guangcheng ameeleza kuwa akiendelea kuishi nchini China masuala yote ya kisheria yanakuwa chini ya taifa hilo kwa hiyo ni wazi ataendelea kukutana na wakati mgumu na kubanwa asifanye shughuli zake kwa uhuru unaostahili.

Mwanaharakati huyo mwenye ulemavu wa macho anaendelea kupata matibabu katika Hospital ya Beijing akiwa chini ya ulinzi imara wa Maofisa wa Marekani kitu ambacho amesema kimempa ahueni kuhusiana na usalama wake pamoja na familia yake.

Kuachiwa kwa Guangcheng ambaye alikuwa anapatiwa hifadhi na Ubalozi wa Marekani baada ya kukimbia kifungo cha ndani kumefanikishwa na ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton.

Clinton ambaye bado yupo ziarani nchini China ameitaka nchi hiyo kuheshimu haki za binadamu na kuachana na tabia za kuwakandamiza Wanaharakati pale ambapo wanakosoa utendaji wa serikali.

Serikali ya Beijing ilikuwa mbogo na kuishutumu Marekani kutokana na kuingilia masuala yake ya ndani kutokana na wao kulazimisha Guangcheng aachiwe licha ya makosa ambayo ameyatenda.

Guangcheng alikumbana na kifungo cha nyumbani baada ya kukosoa sera mpya ya serikali ambayo inataka kuhalalisha utoaji wa mimba na kutaka kila mtu azae mtoto mmoja ili kukabiliana na ongezeko la watu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.