Pata taarifa kuu
Sudani-Sudani Kusini

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa UN alaani mashambulizi ya ndege za Sudani mpakani na Sudani kusini

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amelaani vikali mashambulio ya ndege za Sudan Kwenye mpaka wake na jirani yake Sudan Kusini na kuwataka viongozi wa nchi hizo mbili kuketi kwenye meza ya mazungumzo ili kumaliza tofauti zao.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Un Ban Ki Moon
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Un Ban Ki Moon
Matangazo ya kibiashara

Kwa Mujibu wa naibu msemaji wa Umoja wa Mataifa UN Eduardo del Buey., amesema kwamba mbali na kulaani mashambulio hayo Ban Ki Moon ametaka Sudan isitishe mara moja mashambulio akiongeza kuwa harakati za kijeshi kamwe haziwezi kusuluhisha mzozo wa mipaka kati ya nchi hizo mbili.

Ban Ki Moon amewatolea wito ma rais Salva Kiir na Omar Al Bashir, kuacha uhasama, badala yake waketi kwenye meza ya mazungumzo ili kumaliza tofauti zao, na walichukulie jambo hili kama la dharula, linalo hitaji kupatiwa suluhu haraka iwezekanavyo.

Wito huu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kutaka mazungumzo baina ya nchi hizo mbili unatokea baada ya ya rais wa Sudan Omar Hassan Al Bashir kutupilia mbali pendekezo la kuketi kwenye meza ya mazungumzo na jirani yake wa Kusini Salva Kiir, na ambae kwa sasa anazuru nchini Uchina kutafuta uungwaji mkono.

Ndege za kijeshi za Sudan zilishambulia mji wa Bentiu ulioko Sudan kusini na kusababisha maafa ya raia wa kawaida na hasara kubwa kwenye mji huo.

Hapo jana rais wa Sudani alitembelea eneo la mzozo la Heglig lililokuwa limetekwa na wanajeshi wa Sudani Kusibi na kuwaambia wanajeshi wake kwamba muda wa mazungumzo na Sudani Kusini umekwisha.

Sudani Kusini iliondowa vikosi vyake katika eneo la mzozo la Heglig, lakini serikali ya Khartoum inasema kwamba wanajeshi hao walitimuliwa kwa nguvu za kijeshi.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.