Pata taarifa kuu

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa la laani mapinduzi ya kijeshi nchini Guinea Bisau

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UN kwa kauli moja hapo jana limeazimia na kulaani mapinduzi ya kijeshi yaliyofanyika nchini Guinea-Bissau na kutaka utawala wa kiraia urejeshwe, na waachwe huru viongozi walitiwa nguvuni akiwemo waziri mkuu wa nchi hiyo Carlos Gomez Junior.

Baraza la Bunge nchini Guinea Bisau
Baraza la Bunge nchini Guinea Bisau © Alfa Bade/AFP
Matangazo ya kibiashara

Juma lililopita Umoja wa Afrika AU ulipitisha azimio la kuifuta uanachama kwa muda nchi hiyo na kuagiza utawala wa kijeshi nchini humo kurejesha katiba ya nchi na kuruhusu utawala wa kiraia.

Hapo jana rais wa kikao cha baraza la usalama la umoja wa mataifa UN Suzan Rice aliwataka wanajeshi hao kuwaachilia huru rais wa mpito, waziri mkuu na viongozi wengine wa serikali na kuwataka waheshimu haki za binadamu.

Utawala wa kijeshi nchini humo umetangaza kuwa utakaa madarakani kwa muda wa miaka miwili wakati ikijiandaa kufanya uchaguzi mkuu wa urais, hatua mabayo imepingwa vikali na nchi wanachama za ECOWAS na umoja wa Afrika AU.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.