Pata taarifa kuu
SUDAN-SUDAN KUSINI

Khartoum yaitangaza nchi ya Sudan Kusini kama taifa adui kwa usalama wake

Bunge nchini Sudan limepiga kura ya kuidhinisha jirani zao wa Sudan Kusini kama Taifa adui kwao wakati huu ambapo serikali ya Khartoum ikikanusha madai ya kushambulia Kambi ya Umoja wa Mataifa UN iliyopo Juba. 

Mwanajeshi wa Sudan Kusini akiwa kwenye doria jimboni Heglig
Mwanajeshi wa Sudan Kusini akiwa kwenye doria jimboni Heglig Reuters
Matangazo ya kibiashara

Wabunge nchini Sudan chini ya Spika wa Bunge Ahmed Ibrahim El-Tahir amesema kwa sasa wametangaza vita na SPLM hadi pale ambapo serikali ya Sudan Kusini itakapoliachia eneo lenye utajiri wa mafuta la Heglig walilolitwaa baada ya kuwasambaratisha wanajeshi wa Sudan.

Hatua hiyo ya Sudan imefikiwa wakati pia baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likizitaka nchi hizo mbili kumaliza tofauti zao za kimipaka kwa lengo la kuleta amani kwenye maeneo yenye mgogoro.

Lakini wakati Khartoum ikitangaza kuwa Sudan Kusini ni adui yake, serikali ya Juba yenyewe imeendelea kusisitiza kutoondoa vikosi vyake kwenye jimbo la Heglig ambalo ndilo chanzo cha mapigano kati ya mataifa hayo mawili.

Hali katika eneo hilo imeendelea kuwa tete kila uchao kutokana na kuongezeka kwa mashambulizi yanayofanywa na majeshi ya Sudan kwenye jimbo hilo lenye utajiri wa mafuta.

Jumuiya ya kimataifa ikiwemo Umoja wa Afrika umetakiwa kuingilia kati mgogoro huo kabla haujazusha vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya mataifa hayo mawili hasimu ambapo uhasama umeongezeka tangu Sudan kusini kujitenga.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.