Pata taarifa kuu
MALI

Viongozi wa serikali ya kijeshi nchini Mali imekubali mpango wa kukabidhi madaraka

Viongozi wa serikali ya kijeshi nchini Mali na mataifa jirani wamefikia makubaliano ya mpango wa kuachia madaraka ili kusamehewa vikwazo vya biashara na diplomasia.

Kiongozi wa serikali ya kijeshi nchini Mali,Amadou Sanogo
Kiongozi wa serikali ya kijeshi nchini Mali,Amadou Sanogo REUTERS/Luc Gnago
Matangazo ya kibiashara

Jeshi la Junta nchini Mali na nchi za Afrika magharibi Ecowas walitangazia umma mpango huo kupitia kituo cha televisheni siku ya ijumaa.

Mpango huo ulitiwa sahihi na wapatanishi na kiongozi wa serikali ya jeshi kapteni Amadou Sanogo tayari kwa jeshi hilo kukabidhi spika wa bunge Dioncounda Traore ambaye aliapa kuwa raisi wa mpito lengo likiwa kusimamia harakati za uchaguzi nchini humo.

Mpango huo pia unahusisha kutupilia mbali vikwazo vya Ecowas na kutoa msamaha kwa wale walioshiriki katika mapinduzi ya kijeshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.