Pata taarifa kuu
THAILAND

Chanzo cha moto katika hoteli ya Lee Gardens chafahamika.

Uchunguzi uliofanywa kuhusu tukio la moto lililotokea katika hotel ya Lee Gardens nchini Thailand hapo jana, umebainisha kuwa moto huo ulisababishwa na mlipuko wa bomu lililokuwa limetegwa garini na watu wanaohofiwa kuwa waasi kwa mujibu wa taarifa ya mkuu wa polisi nchini humo iliyotolewa kupitia television.

rt.com
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na kupitiwa upya kwa takwimu za maafa yaliyosababishwa na moto huo,takwimu mpya zilizotolewa na gavana wa jimbo zimebainisha kuwa watu watatu wamepoteza maisha akiwemo mtalii kutoka nchini Malaysia na kujeruhi mamia wengine

Hapo jana Gavana wa jimbo la Songkhal katika mji wa Hat Yai ameliambia shirika la habari la AFP kuwa wanaume wanne na mwanamke mmoja wameuwawa na kuteketea katika moto ambapo watu 336 wamejeruhiwa na kwamba watu 28 kati yao wamepelekwa hospitalini kwa matibabu zaidi.

Tukio hilo limetokea sambamba na tukio lingine la shambulio la bomu ambalo limeua watu kumi katika maeneo mbalimbali ya ukanda huo.
Β 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.