Pata taarifa kuu
MALI-ECOWAS

Viongozi wa ECOWAS wabadili mpango wa mazungumzo jijini Bamako

Ujumbe wa viongozi wa Afrika Magharibi umebadili mpango wake wa kuelekea nchini Mali kujadiliana na viongozi wa mapinduzi ya wiki iliyopita. Duru kutoka ikulu ya rais ya nchini Cote d'Ivoire zaarifu kuwa badala ya mkutano huo kufanyika nchini Mali, mazungumzo hayo yatafanyika jijini Abijan.

Viongozi wa ECOWAS katika kikao chao jijini Abijan machi 28.
Viongozi wa ECOWAS katika kikao chao jijini Abijan machi 28. REUTERS/Thierry Gouegnon
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo duru kutoka shirika la Habari la AFP zaarifu kuwa uamuzi huo umekuja baada ya maandamano ya watu wanaounga mkono mapinduzi kuvamia uwanja wa ndege katika eneo la kupaa na kutua ndege. Habari zaidi zinaarifukuwa ndege iliokuwa ikiwasafirisha viongozi hao, ilikuwa tayati katika anga la Mali karibu kutuwa.

Nchi jirani ya Mali zimewatahadharisha wanaounga mkono mapinduzi hayo kukaa pembeni, na tayari majeshi ya amani yamewekwa katika hali ya tahadhari.

Hapo jana Jumatano maelfu ya watu waliandamana mitaani kuunga mkono mapinduzi hayo.Wengi walikasirishwa na kile wanachokiita uingiliaji wa maswala ya Mali na nchi za kigeni.

Viongozi wa mapinduzi wametoa maelezo ya katiba mpya pamoja na kutangaza tarehe ya uchaguzi ambapo wale waliohusika na mapinduzi hawataruhusiwa kushiriki ingawa tarehe halisi haijatangazwa bado.

Mapinduzi yaliongozwa na askari ambao hawakufurahishwa na jinsi serikali ya Toure ilivyokuwa ikishughulikia suala la waasi wa Tuareg kaskazini mwa nchi.
Waasi wa Tuareg wameliviondoa vikosi vya jeshi katika miji kadhaa ya kaskazini katika miezi ya hivi karibuni.

Chini ya katiba mpya kamati ya mpito yenye wajumbe 26 kutoka vikosi vya usalama na raia 15 watashirika madaraka. Wale watakaofanya kazi katika kamati hiyo wamepewa kinga ya kushtakiwa.

Baadhi ya nyaraka katika katiba hiyo zinafanana na katiba ya sasa yaMali zikiwemo uhuru wa kujieleza, mawazo na kutembea.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.