Pata taarifa kuu
MALI

Wanajeshi walioasi nchini Mali wasema viongozi wa serikali waliotiwa mbaroni wako salama.

Kiongozi wa jeshi lililoasi nchini Mali Amadou Sanogo amesema rais Amadou Toumani Toure yuko salama pamoja na maafisa wengine wa serikali waliokamatwa na watafikishwa Mahakamani, wakati Ufaransa ikisema imeshindwa kuwasiliana na rais Toure.

Matangazo ya kibiashara

Jumuiya ya Kimataifa imeendelea kulaani mapinduzi yaliyofanywa na wanajeshi waasi nchini Mali na kufunga mipaka, kusitisha katiba na kuvunja taasisi mbali mbali za serikali.

Taarifa iliyotolewa na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa imelaani vikali tukio hilo la kuchukua madaraka kwa nguvu za kijeshi kutoka kwenye serikali iliyochaguliwa na watu kidemokrasia.

Baraza hilo limetoa wito kwa waasi hao kuhakikisha kunakuwa na usalama wa kutosha kwa wananchi na rais aliyng'olewa madarakani Amadou Toumani Toure huku waasi hao wakisema wamechukua hatua hiyo baada ya serikali kushindwa kukabiliana na waasi wa Tuareg.

Aidha,Jumuiya ya kimataifa inataka uchaguzi wa urais kufanya nchini humo haraka iwezekanavyo ili kumaliza uongozi huo wa kijeshi na uongozi wa nchi hiyo kuongozwa kwa misingi ya sheria na maafisa wote wa serikali waliokamatwa kuachiliwa huru.

Kundi hilo la kijeshi chini ya Luteni Kanali Amadou Konare, limesema serikali ya Mali kwa sasa haina uwezo wa kuwalinda raia wake na kupambana  na ugaidi.

Kiongozi wa jeshi hilo la waasi hata hivyo, aliongeza kuwa baada ya kurejea kwa usalama nchini humo uongozi wa kiraia utarejea mamlakani.

Ripoti zinaeleza kuwa, rais Amadou Toumani Toure ambaye alikuwa amejificha Ikulu alifaulu kutoroka baada ya mashambulizi kuanza kushuhudiwa nje ya Ikulu na kwa sasa rais huyo anaelezwa kuwa katika kambi ya jeshi.

Kupinduliwa kwa rais Toure kumetokea siku kadhaa kabla ya  kujizulu kwake, wakati  uchaguzi mkuu nchini humo ukitarajiwa mwezi ujao wa nne.

Rais Toure aliingia madarakani kwa mapinduzi kabla ya kurejesha utawala mikoni mwa raia, na baadae kuchaguliwa kwa mihula miwii tangu mwaka wa 2002.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.