Pata taarifa kuu
SYRIA-UN

Majeshi ya Syria yavamia wapinzani,rais Asaad ashinikizwa kutekelekeza mapendekezo ya Annan

Majeshi ya serikali nchini Syria yanaendeleza uvamizi dhidi ya wapinzani katika ngome zao ikiwemo mkoa wa Idlib na mjini Daraa,hata baada ya baraza la usalama la umoja wa mataifa kumtaka rais Bashar Al Asaad kuridhia mapendekezo ya mjumbe wa amani wa Umoja huo Koffi Annan kuhusu namna ya kumaliza machafuko yanayoendelea.

Matangazo ya kibiashara

Nao wanajeshi waasi wametangaza kuwa wamebuni baraza la kuendeleza oparesheni zao mjini Damacus.

Kanali Khaled Mohammed al -Hammud anatoa wito kwa wanajeshi wengine ambao wako katika serikali ya rais Asaad kujiunga nao ili kuendeleza mapambano dhidi ya uongozi wake.

Kuafikiana kwa wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuwa rais Asaad aridhie mapendekezo ya Koffi Annan, au atachuliwa hatua zaidi kunaelezwa na wanaharakati nchini humo kuwa ni ishara kuwa kuna matumaini ya Asaad kusalimu amri na kuondoka mamlakani lakini wanataka hatua zaidi kuchuliwa dhidi ya rais huyo.

Koffi Annan anatarajiwa kurudi Damascus hivi karibuni kufanya mazungumzo zaidi na rais Bashar Al Asaad na viongozi wa upinzani na kuthamini kuhusu mapendekezo sita  aliyotoa kwa pande hizo mbili.

Mazungumzo ya Annan na viongozi wa upinzani yanalenga kusitisha mapigano yanayoendelea kwa sasa kabla ya kuanza mazungumzo ya kuleta maridhiano ya kisiasa nchini humo na pia kuwasaidia waathiriwa wa mapigano hayo kwa misaada ya kibinadamu.

Annan amekuwa akitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuzungumza kwa sauti moja dhidi ya mapigano nchini Syria na kuunga mkono juhudi zake za kupata suluhu.
Tayari msuluhishi huyo amekutana na rais Bashar Al Asaad na viongozi wa upinzani mapema mwezi huu na kutoa mapendekezo anayosema yatasaidia kumaliza mzozo huo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.