Pata taarifa kuu
NIGERIA-UINGEREZA

Nigeria yaanza mahojiano na watuhumiwa wa utekaji nyara raia wa uingereza.

Watuhumiwa wa utekaji nyara uliofanywa kwa raia wawili wa bara la ulaya wameanza kuhojiwa juu ya utekaji uliotokea wakati wa zoezi la uhamisho kwa raia wa uingereza na nigeria jambo ambalo hivi karibuni limesababisha kutofautiana kati ya Italia na Nigeria.

Watuhumiwa wa utekaji nyara nchini Nigeria waanza kuhojiwa kufuatia kuteka nyara na kuua raia wawili wa barani Ulaya.
Watuhumiwa wa utekaji nyara nchini Nigeria waanza kuhojiwa kufuatia kuteka nyara na kuua raia wawili wa barani Ulaya. AFP PHOTO/ANI
Matangazo ya kibiashara

Mhandisi kutoka Italia Francesco Molinara, aliyekuwa na umri wa miaka 48, na mwenzake raia wa uingereza Chris McManus,umri wa miaka 28, walisadikika kuuawa kwa kupigwa risasi na watekaji hao kabla ya kuokolewa.

Vyanzo kutoka kwa majeshi ya usalama nchini Nigeria vimearifu kuwa watuhumiwa nane wamesafirishwa kulelekea Abuja ambapo walikiri kuhusika na mauaji yaliyotokea katika mji wa sokoto wakati wa zoezi la uhamisho.

Chanzo kimoja kilisema wanaendelea na mahojiano na watuhumiwa hao ili kupata tukio kamili la yaliyotokea ndipo watatoa taarifa kamili.

Wakati huo huo Italia imelaani Uingereza kushindwa zoezi la uokoaji jambo ambalo Uingereza imejitetea kuwa hali ya mambo haikuwataka kutenda kwa pupa.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.