Pata taarifa kuu
SYRIA

Raia nchini Syria wapiga kura ya maoni kuhusu katiba mpya.

Kura ya maoni kuhusu katiba mpya inapigwa nchini Syria hii leo, ingawa ghasia zimeripotiwa kuendelea nchini humo huku wapinzani wakitoa wito kwa raia kususia kura hiyo. 

kiswahili.rfi.fr
Matangazo ya kibiashara

Kura hiyo ni muhimu katika kuleta mabadiliko yaliyopendekezwa na Rais Bashar al-Assad nchini humo ambapo katiba mpya itaruhusu mfumo wa vyama vingi

Uamuzi wa kuitisha kura ya maoni umekuja kwa lengo la kuwatuliza wapinzani wa serikli ya rais Bashar Al Assad ambao wanamtaka rais huyo kuondoka madarakani.

Hata hivyo haijulikani iwapo kura hiyo ya maoni itafananikiwa ikiwa bado machafuko yanaendelea nchini humo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.