Pata taarifa kuu
Syria-Ufaransa

waandishi wa habari wawili wa kigeni wauawa nchini Syria

Waandishi wa habari wawili wameuawa jijini homs jumatano hii Februari 22 wakiwa katika kituo cha uandishi habari katika kata ya Baba Amr. Waandishi hao mmoja ambae ni mpiga picha raia wa Ufaransa Rémi Ochlik, na mwingine ni raia wa Marekani Marie Colvin ambae alikuwa anatumikia gazeti la Sunday Times wameuawa baada ya kushambuliwa na makombora ya jeshi la Syria

Syria baba Amir jijini Homs
Syria baba Amir jijini Homs REUTERS/Handout
Matangazo ya kibiashara

Kombora lililorushwa na jeshi la Syria, liliwajeruhi vibaya waandishi hao wawili wakati walipokuwa wakijaribu kukimbia. Waandishi wa habari wengine wa kimataifa wamejeruhiwa akiwemo muandishi wa habari mwengine wa Ufaransa

Habari za kifo cha Rémi Ochlik mwenye umri wa miaka 28 na mwenzie Marie Colvin zimethibitishwa na viongozi wa Ufaransa kupitia waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Alain Juppe. Mwanaharakati wa Syria akiwa kwenye eneo la tukio amesema wanajaribu kutowa miili ya waandishi hao wa habari lakini kuna uzito mkubwa. Jiji la Homs linashuhudia mashambulizi yasiokoma ya jeshi la Syria wiki tatu sasa.

Rémi Ochlik mshindi wa tuzo la World Press Photo alikuwa amerejea nchini Syria mwishoni mwa juma lililopita ambapo katika risala yake ya jana Februari 21 alifahamisha kuhusu hali halisi ilivyo jijini Homs. Mwenzie Marie Colvin anajulikana kutokana na ripoti zake katika maeneo ya mizozo ya kivita ambapo alifaanikiwa kupewa tuzo la mwanaripota bora wa maeneo ya mizozo ya kivita katika mwaka 2010 nchini Uingereza.

 

Rémi Ochlik ni muandishi wa habari wa pili wa Ufaransa kuuawa nchini Syria katika jiji la Homs. Mfaransa mwingine Gilles Jacquier aliuawa Januari 11 jijini Homs jiji ambalo linachukuliwa kama kitovu cha maandamano ya kumpigan rais Bashar Al Assad.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.