Pata taarifa kuu
Iran-Nyuklia

Iran yandelea kusisitiza kuhusu mpango wake wa kurutubisha nyuklia

Licha ya kuwasili nchini Iran kwa waangalizi wa shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia nguvu za Atomic duniani IAEA, serikali ya nchi hiyo imesema kuwa mpango wake wa kurutubisha nyuklia kwaajili ya matumizi ya kijamii uko palepale.

Rais wa Iran Mahmoud Ahmadinejad wakati wa sherehe za uzinduzi wa mpango wa nyuklia wa Iran Februari 15, 2012
Rais wa Iran Mahmoud Ahmadinejad wakati wa sherehe za uzinduzi wa mpango wa nyuklia wa Iran Februari 15, 2012 Reuters / President.ir
Matangazo ya kibiashara

Msemaji katika wizara ya mambo ya nje ya Iran Ramin Mehmanparast amesisitiza nchi yake kutobadili msimamo wake wa matumizi ya Nyuklia kwa aajili ya kijamii licha ya mazungumzo ambayo yanaendelea kati ya nchi yake na waangalizi wa Umoja wa Mataifa.

Ikulu ya Tehran imekuwa katika mvutano wa maneno na mataifa ya magharibi kufuatia mataifa hayo kuendelea kuongeza vikwazo zaidi kwa nchi hiyo kufuatia kuendelea na mpango wake wa kurutubisha matumizi ya Uranium ambayo nchi hiyo imekuwa ikituhumiwa kutengeneza silaha za maangalizi.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.