Pata taarifa kuu
BRUSSELS

Sheria ya kubana matumizi yatarajiwa kuwa ajenda kuu ya mkutano wa viongozi wa EU mjini Brussels

Viongozi wa Umoja wa ulaya hii leo wanaanza mkutano wao wa kiuchumi mjini Brussels Ubelgiji ambapo ajenda kubwa ya mkutano huo inatarajiwa kuwa ni namna ya kutafuta njia zaidi ya kukabiliana na mdororo wa kiuchumi barani Ulaya.

Rais wa Ufaransa, Nikolas Sarkozy
Rais wa Ufaransa, Nikolas Sarkozy REUTERS/Robert Pratta
Matangazo ya kibiashara

Katika mkutano huo viongozi wa nchi wanachama wanatarajiwa kutia saini makubaliano mapya ya kubana bajeti na sheria ya kudhiabu nchi ambazo zitakwenda kinyume na ubanaji wa matumizi, sheria ambayo hata hivyo nchi ya Uingereza haikubaliani nayo.

Sheria hiyo mpya ambayo itazishuhudia nchi za Ufaransa na Ujerumani zikiwa ndio vinara wa kusimamia michakato yote ya ubanaji wa matumizi kwa nchi wanachama, ilizua mzozo mkubwa na nchi ya Uingereza ambayo ilijitoa kwenye mpango huo mpya.

Inakadiriwa kuwa zaidi ya wananchi milioni 23 hawana ajira kwenye Umoja huo, na kuendelea kuzua hofu ya hali ya uchumi kwenye mataifa hayo kudorora zaidi na kufanya hali kuwa mbaya zaidi kuliko ilivyotarajiwa.

Hapo jana rais wa Ufaransa Nikolas Sarkozy alitangaza mikakati mipya ya serikali yake katika kukabiliana hali mbaya ya uchumi kwenye nchi yake na kwamba ataongeza kodi ya mapato kutoka asilimia 19 hadi kufikia asilimia 21 ambayo anaamini itaweza kutengeneza ajira.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.