Pata taarifa kuu
IRAN

Ujumbe wa wakaguzi wa shirika la kimataifa la nguvu za Atomic IAEA umewasili nchini Iran.

Ujumbe wa maafisa wa ngazi za juu wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomic IAEA umewasili nchini Iran, kutafuta njia za kusuluhisha mgogoro kuhusu mpango wa nchi hiyo kuzalisha madini ya uranium.

Mkuu wa shirika la kimataifa la nguvu za Atomic Herman Nackaerts
Mkuu wa shirika la kimataifa la nguvu za Atomic Herman Nackaerts presstv.ir
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa ujumbe huo Herman Nackaerts amesema ana imani Iran itatoa ushirikiano katika kumaliza wasiwasi uliopo kwamba mpango wake wa nyuklia una ajenda za kijeshi.

Mazungumzo baina ya ujumbe huo na maofisa wa Iran yanatarajia kuanza baadaye hii leo hadi siku ya Jumanne ingawa kiongozi huyo amesisisitiza kuwa mazungumzo hayo yalipaswa kuanza zamani.

Iran imekuwa ikikanusha shutuma kuwa mpango wake wa nyuklia una agenda za siri za kuunda silaha za atomiki.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.