Pata taarifa kuu
LIBYA-MAREKANI

Umoja wa Mataifa UN wasema maelfu ya wafungwa nchini Libya wanakabiliwa na mateso

Wafungwa waliokamatwa baada ya kukamilika kwa Mapinduzi ya kuuangusha Utawala wa Kiongozi wa zamani wa Libya Kanali Muammar Gaddafi wameendelea kuteshwa licha ya juhudi kufanyika kuzuia hilo.

REUTERS/Denis Balibouse
Matangazo ya kibiashara

Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa UN limesema wafungwa hao ambao wanaaminika kuwa ni wafuasi wa Marehemu Kanali Gaddafi wameendelea kukabiliwa na mateso makali kwenye magereza wanayoshikiliwa.

Mkuu wa Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa UN Navi Pillay amesema maelfu ya wafungwa nchini Libya wanaendelea kutaabika kutokana na mateso wanayoyapata kwenye maeneo wanayoshikiliwa.

Pillay ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UN wengi wa wafungwa hao ambao wanatuhumiwa kuwa wafuasi wa Marehemu Kanali Gaddafi wanakabiliwa na hali ngumu.

Mkuu wa Shirika la Kutetea Haki za Binadamu amesema taarifa ambazo wafanyakazi wake wanazo ni kuwa vitendo vya utesaji vimezidi kushamiri kwa wafungwa hao ambao wengi wao wanatoka katika nchi za eneo la Sahara.

Pillay amesema kuwa wanataka Wizara ya Sheria nchini Libya na Ofisi ya Mwendesha Mashtaka inawaachia wafungwa hao au kama wakishindwa kufanya hivyo wahakikishe wanashtakiwa kwa kufuata haki.

Maelfu ya wafungwa nchini Libya bado wanashikiliwa na makundi ya wapiganaji ambayo yalisaidia kuangushwa kwa Utawala wa Marehemu Kanali Gaddafi na sasa serikali inahaha kuhakikisha inakabidhiwa wafungwa hao.

Umoja wa Mataifa UN umesema serikali ya Libya inashindwa kuwachukua wafungwa hao kutokana na kukosa wafanyakazi wa magereza nchini humo kitu ambacho kinaweza kikachangia kuendelea kwa mateso hayo.

Tangu kuangushwa kwa serikali ya Marehemu Kanali Gaddafi utawala mpya chini ya Baraza la Mpito la Taifa la Waasi NTC masuala mengi ya kiutawala bado hayajafanyiwa kazi hadi sasa.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.