Pata taarifa kuu
LIBYA

Ofisi za baraza la mpito nchi Libya zashambuliwa

Waandamanaji wenye hasira wamevamia na kufanya vurugu katika ofisi za baraza la mpito NTC huko Benghazi nchini Libya kwa nia ya kudai uwazi na usawa katika serikali hiyo.

Kiongozi wa serikali ya mpito nchini Libya,Mustafa Abdeljalil
Kiongozi wa serikali ya mpito nchini Libya,Mustafa Abdeljalil REUTERS/Esam Al-Fetori
Matangazo ya kibiashara

Shambulizi hilo limefanyika katika eneo la mashariki ambapo waasi walishiriki katika harakati za kuuondoa utawala wa kanamli Gaddafi ndio walihusika na vurugu hizo baada ya kutoridhishwa na utendaji wa serikali hiyo mpya.

Takribani waandamanaji elfu mbili,sambamba na askari waliojeruhiwa katika mapinduzi yaliyotokea mwaka jana wamedai kusahaulika sana baada ya serikali mpya kushika uongozi.

Mashuhuda wamesema waandamanaji walitumia mawe na mabomu ya kienyeji katika kushambulia ofisi hizo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.