Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-MAREKANI

Marekani yatambua wanajeshi wake katika picha za video

Maafisa wa serikali nchini Marekani wanasema wametambua picha za video za wanajeshi wawili wa majini raia wa Marekani wakitoa haja ndogo juu ya miili ya wapiganaji wa kundi la wanamgambo wa Taliban nchini Afghanistan.

Waziri wa ulinzi wa marekani Leone Panneta
Waziri wa ulinzi wa marekani Leone Panneta Reuters/Jason Reed
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa ulinzi wa marekani Leone Panneta amesema picha hizo ni za kweli na amekemea vikali tukio hilo na kusema waliohusika katika tukio hilo watawajibika ipasavyo, kauli iliyoungwa mkono na waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Hillary Clinton.

Tukio hilo linaelezwa kuwa huenda litadhoofisha mazungumzo kati ya Marekani na wanajeshi wa Taliban katika mpango wa kuleta amani nchini Afghanistan.

Hata hivyo msemaji wa majeshi ya muungano ya kimataifa ya NATO nchini Afghanistan Jenerali Carsten Jacobson amesema kuwa marekani itafanya juhudi kuhakikisha kuwa inapinga vikali vitendo hivyo.

Takriban wanajeshi elfu ishirini wako nchini Afghanistan hasa katika jimbo la Kandahar na Helmand kusini mwa nchi hiyo katika juhudi za kulinda amani..
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.