Pata taarifa kuu
RWANDA

Rwanda yaridhishwa na ripoti ya majaji wa ufaransa juu ya mauaji ya 1994

Rwanda inasema imepokea kwa mikono miwili ripoti ya majaji wa Ufaransa waliokuwa wanachunguza kifo cha raia wa zamani wa nchi hiyo Juvenal Habyarimana aliuawa baada ya ndege yake kudunduliwa mwaka 1994 na kusabisha mauaji ya kimbari nchini Rwanda.

Raisi wa Rwanda Paul Kagame
Raisi wa Rwanda Paul Kagame © AFP/Thomas Samson
Matangazo ya kibiashara

Ripoti hiyo imewaondoa washirika wa karibu wa rais Paul Kagame kuhusika na kifo hicho cha Habyarimana tuhuma ambazo wamekuwa wakishutumiwa kwa kipindi kirefu sasa.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa,ndege iliyokuwa imembeba Habyarimana ilidunguliwa na wanajeshi wa Habyarimana wa FAR.

Mtaalamu wa mauaji ya kimbari yalitokea nchini Rwanda Tom Ndahiro nae amesema kuwa ripoti hiyo imejaribu kuelezea uhalisia wa mambo yalivyokuwa na kwa kiasi kikubwa imemwondolea rais Kagame shutuma zilizokuwa zikimwandama.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.