Pata taarifa kuu
IRAN

Jumuia ya kimataifa yatahadharisha juu ya mvutano baina ya mataifa ya magharibi na Iran

Mvutano uliopo kati ya Iran na nchi za magharibi umeleta hali ya tahadhari kuwa Iran inaelekea kuwa nchi ya hatari, huku jumuia ya kimataifa ikitoa tahadhari juu ya mpango wa Iran wa kurutubisha madini ya Uraniam.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani,Hillary Clinton
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani,Hillary Clinton REUTERS/J. Scott Applewhite
Matangazo ya kibiashara

Kitendo cha Iran kutozingatia matakwa ya jumuia ya kimataifa, imefanya Marekani na umoja wa ulaya kuchukua hatua ya kuiwekea zaidi vikwazo vya kiuchumi Iran.

Hatua hiyo ya iran inakuja baada ya shirika la nguvu za atomiki duniani kuthibitisha kuwa Iran imeanza urutubishaji wa madini ya Uranium katika eneo jipya kusini magharibi wa mji wa Tehran.

Hatua hiyo ya Iran imeelezwa na marekani, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani kuwa ni ukiukwaji wa maazimio la baraza la usalama la Umoja wa mataifa, huku marekani kupitia waziri wake wa mambo ya nje Hillary Clinton akiitaka Tehran kusitisha shughuli za urutubishaji.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.